MWANZO  >>  KISWAHILI  
1. Sera na Miongozo
2. Utapiamlo
3. Lishe ya Mama na Mtoto
4. Lishe  & UKIMWI
5. Uwakiki wa Chakula
6. Viashirio vya Lishe
   
   
Sera na Miongozo ya Lishe  

Sera ya Lishe

Jitihada za serikali za kuinua kiwango cha ubora wa huduma za afya na lishe katika jamii zimezingatia mambo muhimu kama vile utoaji wa miongozo ya kisiasa, kupitisha sera mbalimbali, kubuni na kuchukua hatua mahususi zinazolenga katika kuinua hali ya lishe. Sera na hatua hizo zilianza kubuniwa na kutekelezwa mara baada ya kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 na kuimarika zaidi baada ya Azimio la Arusha la mwaka 1967. [bonyeza hapa]


Mwongozo wa Kitaifa Kuhusu Matunzo na Huduma za Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na Wenye Ukimwi.

Hivi sasa tatizo la maambukizo ya virusi vya UKIMWI duniani limekuwa kubwa kuliko ilivyofikiriwa miaka ya nyuma. Nchini Tanzania kiwango cha maambukizo kiko juu, yaani asilimia 9.6 kwa watu wazima.[bonyeza hapa]


Mwongozo wa Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na Wenye Ukimwi

Tatizo la VVU/UKIMWI linaendelea kuwa tishio kwa maisha ya binadamu. Pamoja na jitihada mbalimbali za kitabibu, imeonekana kuwa watu wengi wanaoishi na virusi vya UKIMWI (VVU) au UKIMWI huathirika au hupoteza maisha yao mapema zaidi kwa kukosa lishe bora. [bonyeza hapa]

 
   
   
          Hatimiliki  © 2005 - 2006 Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania | Ushauri na Huduma | Tuwasiliane